WANANCHI WATAKIWA KULINDA MRADI WA MAJI
Wananchi wa Mtaa wa Jangwani Kata ya Chinkonji katika Manispaa ya Lindi, wametakiwa kuusimamia na kulinda mradi wa maji.
Mradi huu maji wa Chikonji ambao una awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa miundombinu ya vyanzo pamoja na ile ya usambaza maji Chikonji Kusini na Kaskazini kwa gharama ya shilingi 1,171,919,650. Awamu ya pili ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji Jangwani na Nanyanje kwa gharama ya shilingi 315,261,408. Awamu ya tatu ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji Mtaa wa Mkanga kwa gharama ya shilingi 483,720,490, hivyo jumla ya fedha za mradi mzima ni shilingi 1,970,901,548.
Haya aliyasema Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Chikonji ambapo katika Mtaa wa Jangwani alikagua shule ya msingi Jangwani na kufanya mkutano na wananchi wa Jangwani.
Mhe. Zambi alilazimika kuyasema haya baada ya kupata malalamiko toka kwa mhandisi wa maji kuwa wananchi wamekuwa na tabia ya kukata mabomba na kudumbukiza vitu ili kukwamisha mradi usikamilike wakati wanayoshida kubwa ya maji.
“Wananchi mradi huu wa maji ni wenu, hivyo mnao wajibu mkubwa sana wa kuulinda. Serikali inajenga mradi na ukishakamilika inaukabidhi kwenu ili muuendeshe kupitia kamati yenu ya maji ambayo wajumbe wake mnawachagua wenyewe”, aliesema Mhe. Zambi.
Katika mkutano wa hadhara, alipata lalamiko la ubovu wa barabara ambapo alimuagiza Meneja wa TARURA kuhakikisha anaingiza barabara ya Muhimbili-Jangwani na Jangwani-Chikonji kwenye mpango wa bajeti ya mwaka 2018/2019 lakini halmashauri iangalie kama itapata fedha zozote itengeneze barabara hizi.
Pia alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha katika bajeti ya 2018/2019 wanaingiza ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule ya msingi Jangwani. Aidha, Mhe. Zambi aliagiza choo cha walimu cha kudumu kijengwa na kukamilika ifikapo Decemba, 2017.
Baada ya kumaliza kuongea na wananchi wa Mtaa wa Jangwani, Mhe. Zambi alitembelea mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone – Mingoyo ambapo alimtaka kuhakikisha anawapelekea mbegu wanakikundi ili shughuli za kilimo zeweze kuanza.
Aidha, alifanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Nachingwea ambapo alisikiliza kero mbalimbali za wananchi huku kero kubwa ikiwa ni utaratibu mbovu wa ugawaji wa viwanja vilivyopo Mtaa wa Mlandege.
Mhe. Zambi baada ya kusikiliza maelezo kutoka pande zote za viongozi wa Kata na wanachi, alibaini kuwa kulikuwa na mapungufu katika ugawaji wa viwanja na kumuagiza Katibu Tawala Wilaya ya Lindi, Ndg. Thomas Safari ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Lindi kuhakikisha anaunda tume itakayofanya kazi kwa mwezi mmoja kupitia upya taratibu zilizotumika kugawa viwanja.
Aidha, aliagiza kuwa wale wote waliopewa viwanja ambao hawajajenga wasijenge kwani inaonekana wazi kuwa wapo wananchi waliostahili kupewa maeneo hayo na hawajapewa badala yake wanatafutiwa eneo jingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.