Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa Wasimamizi wa Maghala kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu ili kuhakikisha mazao ya wakulima yanayohifadhiwa katika maghala hayo yanaingia na kutoka yakiwa ujazo unaolingana ili kuvutia wafanyabiaashara wa ndani na nje kutumia Mfumo huo.
Vilevile Waziri Jafo ameendelea kuwasisitiza Wakulima kuhifadhi mazao yao katika mfumo wa stakabadhi za ghala yakiwa na ubora na kuacha tabia ya kuchanganya mazao hayo na mazao mengine au mchanga hali inayosababisha mazao hayo kushindwa kuuzika katika soko la kimataifa na kuchafua taswira ya nchi ya Tanzania ambayo imeingia mikataba ya biashara baina ya nchi Jumuiya za Kikanda na Kimataifa
Waziri Jafo, ameyasema hayo Septemba 20, 2024 alipokagua, kuweka Jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuongea na Wananchi wakati wa Ziara Maalum katika Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone" iliyoanza tarehe 17 - 21/09/2024 Mkoani humo.
Aidha, akiwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo, Waziri Jafo, alikagua ujenzi wa Mradi wa Usambazaji Maji unaujumisha Vijiji 56 vya Wilaya ya Ruangwa, Lindi na Nachingwe kutoka chanzo cha mto Nyangao (wilaya ya Lindi) na Ujenzi wa Barabara ya Mipingo yenye urefu wa Km. 0.78 pamoja na Chuo cha Ufundi Stadi VETA, na kuzindua Mradi wa Jengo la ghorofa lenye madarasa 8, ofisi 4 na matundu 24 ya vyoo katika Shule ya Msingi Likangara
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itasimamia itekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa ilinkuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo Wilayani humo inakamilika kwa wakati na kuanza kitoa huduma kwa wananchi katika muda uliopangwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.