Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imekutana na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kufanya nao kikao cha kujifunza kuhusu majukumu ya mamlaka na umuhimu wa bima kiujumla.
Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti wa masoko na Maendeleo TIRA Bwana. Samwel Mwiru amesisitiza kuona umuhimu wa kukata bima mbalimbali ikiwemo bima za nyumba na vyombo vya moto wanavyotumia kusafiria.
"Katika kipindi hiki ambacho serikali inaelekea katika utekelezaji wa adhima ya kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na bima itakayomsaidia pindi apatapo majanga hususan ya ugonjwa, ni muhimu sana kwetu watumishi kuwa na bima ili kujikinga na madhara mbalimbalit yanayojitokeza pindi tupatapo majanga au dharula" ameeleza bwana. Mwiru.
Aidha, amewataka watumishi kuwa na tabia ya kuhakikisha vyombo vya moto wanavyovitumia kama vimekatiwa bima ili kujihakikishia usalama na kulipwa fidia pindi wanapopata majanga kama vile ajali.
Akimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omari, Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Rasilimali watu Bwana. Nathal Linuma ametoa shukrani kwa TIRA kwa kuwapa elimu ya bima watumishi na kuwasisitiza watumishi kuwa mabalozi wazuri kwa kutumia elimu hiyo kuwapa taarifa wananchi juu ya umuhimu na faida za bima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.