Waziri wa maji Mhe. Juma Awesu ametoa pongezi kwa viongozi na wasimamizi wa maji wa Mkoa wa Lindi kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kutekelezwa katika wilaya za mkoa wa lindi.
Waziri Awesu ametoa pongezi hizo jana alipofika na kufanya kikao kidogo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa mkoani Lindi, taarifa ambayo ilisomwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemenga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
“Nitumie nafasi hii kuwapongeza watendaji wetu kwa kazi kubwa wanayoifanya, utekelezaji wa miradi ya maji hauna sababu ya kuwa siri ,jamii ipo ukiishirikisha utafanikiwa, Luwasa ya Lindi mjini hongereni sana mnafaya kazi nzuri ” amesema Mhe. Awesu .
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa upande wa Wilaya ya Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga, amesema miradi mingi ipo kwenye utekelezwaji ambapo aliainisha baadhi ya miradi ambayo utelezwaji wake umekamilika kwa zaidi ya silimia 90%.
“ Tuna mradi wa maji maeneo ya Mitwero, Kitunda na Mkwaya maeneo ambayo yapo pembezoni na vyanzo vya maji………mwanzoni ilikuwa tuutekeleze kwa bilioni takribani 6.8, wenzetu hawa walikaa chini wakachambua wakasema tunaweza kufanya kwa force akaunti ikashuka mpaka bilioni 3.6 kwa hiyo ule mradi umekamilika kwa asilimia 98% na tunatarajia kuukamilisha hivi karibuni, lakini pia tuna mradi wa Ng’apa, Kiduni ,Mayani na Ngongo wa milioni 608 ambao tumekamilisha kwa 100% na maji yanatoka.”
Aidha Mhe. Ndemanga aliainisha miradi mingine inayoendelea ambayo ni miradi ya maji ya Mitwero Mchinga, Nyangao Mtama, pamoja na mradi wa Lindi Ruangwa ambao unafanyika ili kupeleka maji kutoka wilaya ya Lindi kwenda wilayani Ruangwa.
Waziri Awesu yupo ziarani mkoani Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika Wilaya za Ruangwa na Liwale ambapo miradi hiyo inatekelezwa kwenye taasisi za VETA na vituo vya afya ili kuhakikisha taasisi hizo zinapata huduma hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.