Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Ikulu (kazi maalum) Mhe. George Mkuchika amewahimiza watanzania kupenda kula na kunywa bidhaa za korosho kwani zina virutubisho vingi vya kupambana na magonjwa .
Mhe. Mkuchika ametoa Rai hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi, wadau na wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa maadhimisho ya siku ya kula na kunywa bidhaa za korosho ambayo ni mahususi kwa ajili ya uhamasishaji wa ulaji na unywaji wa bidhaa korosho.
Amesema ulaji wa korosho licha ya kumlinda Mlaji dhidi ya magonjwa pia ni husaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Soko la ndani .
"Kwa upande wa afya ya Binadamu ukila korosho zilizobanguliwa unakuwa na faida ya kuzuia ugonjwa wa moyo kwa kuzuia shinikizo la damu, ukila korosho unaongeza viini lishe vinavyozuia hatari vya kupata ugonjwa wa kansa pamoja na kuzuia hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari"
Kaimu mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI- Naliendele Dr. Rashid Kidunda amesema licha ya Mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara kuwa ni wazalishaji wakubwa wa zao la korosho hivyo kuendelea kuwa zao kubwa la kibiashara katika kuchangia kipato cha wakulima hasa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma ni asilimia 10 pekee ya korosho zinazopatikana ndizo hutumika kwa matumizi ya chakula miongoni mwa wanajamii hao.
Kaimu mkurugenzi wa Bodi ya korosho Reveliani Ngaiza amesema zao la korosho ni zao la kipekee tofauti na mazao mengine kwa kuwa Lina matumizi mengi kuanzia kwenye Majani, Mbegu, Tawi , shina na hata mzizi wake
"Ukiacha ulaji wa korosho zao la korosho kwa upande wa Majani yanatumika kama Dawa kutibu minyoo tumboni, kuzuwia kuhara,kutoa Gesi tumboni pamoja na kutibu vidonda vya tumbo"
"KULA KOROSHO KWA AFYA YAKO"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.