Leo akizindua jengo la Chuo Kikuu Huria tawi la Lindi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amepokea jumla ya madawati 1000 kutoka Benki ya EXIM kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa shule za msingi Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Mbeya na Tanga.
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa wa Benki ya EXIM Jaffari Matindu amesema kuwa Mkoa wa Lindi ulitakiwa upatiwe madawati 100 lakini kwa heshima ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack yametolewa jumla ya madawati 200 kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoani Lindi.
Waziri Mkuu akizindua kampeni ya usambazaji madawati hayo ameipongeza Benki ya EXIM kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan huku akizitaka Benki zingine kuiga mfano huo wa maendeleo.
Mhe. Waziri Mkuu katika ziara zake ameendelea kusisitiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule ili wapate elimu kwa ajili ya maendeleo yao na kuwaonya watakaoshindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Sanjali na hilo, Mhe. Waziri Mkuu amewaonya vijana wa kiume kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.