Leo Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji Mkoani Lindi utakaonufaisha vijiji 34 vya Wilaya ya Ruangwa na Vijiji 21 vilivyopo Wilaya ya Nachingwea.
Hafla hiyo imefanyika Leo katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA kilichopo kijiji cha Nandagala, Wilaya ya Ruangwa.
Mradi wa maji ambao umesainiwa Leo Kati ya Wakala wa Maji na Usafi Vijiji, RUWASA na Wakandarasi wawili wa ndani ambao ni M/STC Construction Company Limited na M/S. Emirates Builders Construction Limited unaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa cha changamoto ya upatikanaji maji Safi na salama kwa wananchi wa Wilaya za Nachingwea na Ruangwa.
Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Tsh. bilioni 119.15 ni moja ya Miradi michache mikubwa inayotekelezwa na wakandasi wa kitanzania.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa mradi huu ambao utaanzia kwenye chanzo cha maji kilichopo kijiji cha Nyangao , Wilaya ya Lindi utatekelezwa na Wakandarasi wawili ili kuharakisha upatikanaji wa huduma ya maji Safi na salama kwa wananchi wa Ruangwa na Nachingwea ndani ya muda mfupi.
Mhe. Majaliwa Ameipongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, RUWASA kwa kufanikisha kila kjiji cha Wilaya ya Ruangwa kupata kisima cha maji ingawa changamoto kuwa maji ya visima hivyo yana chumvi. Hivyo kukamilika kwa mradi huu utaondoa kadhia ya wananchi kuzunguka na baiskeli, boda boda kutafuta maji yasiyo na chumvi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Ndg. Clement Kivegalo amewaeleza wananchi kuwa mradi huo unaotoka kwenye chanzo cha maji cha uhakika utakapokamilika utafikia lengo la kitaifa la upatikanaji wa maji Safi na salama kwa asilimia 85.
Ndg. Kivegalo ameendelea kusema kuwa kutokana na uwepo wa maji ya kutosha kwenye chanzo kilichopo katika kijiji cha Nyangao, mradi huu utaweza kuduma zaidi ya miaka 20.
Kwa upande wao, wananchi wa Ruangwa akiwemo Mariam Hamisi Chitanda kutoka kijiji cha Namahema, Wilaya ya Ruangwa wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mradi huu mkubwa utakaoondoa changamoto ya ndoa nyingi kuvunjika Kwa sababu ya kutafuta maji.
Wananchi hao wameongeza kuwa kwa furaha waliyonayo wako tayari kujitolea kufanikisha ujenzi wa mradi huo kuanzia hatua ya mwanzo mpaka kukamilika kwake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.