Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo mchana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Nachingwea amewapongeza wananchi wa kijiji cha Chiumbati kwa kutoa zaidi ya hekta 24 bure kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Akizungumza na wananchi hao Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema wananchi wa Chiumbati ni mfano wa kuiga kwani mbali na kutoa ardhi hiyo lakini wamechangia pia nguvu kazi yenye dhamani ya Tsh. 128,237,810.
Shule ya Sekondari ya wavulana Nachingwea inajengwa na Halmashauri ya Nachingwea ambapo kwa awamu ya kwanza tayari Halmashauri imetumia jumla ya Tsh. 516,983,000 iliyotokana na mapato ya ndani, Tsh. 40,000,000/= kutoka EP4R pamoja na nguvu za wananchi. Ujenzi wa shule hii unatarajiwa kumalizika mwaka 2024 utagharimu jumla ya bilioni 4.5.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack licha ya kupongeza ujenzi wa shule hiyo lakini pia amefurahishwa na ubora wa majengo yanayojengwa chini ya Muhandisi mwanamke na kuahidi kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa shule hiyo pamoja na miradi yote ya serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.