Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo akizungumza na wananchi wa kata ya Naipanga Wilaya ya Nachingwea alipotembelea mradi wa ujenzi wa zahanati ameeleza sababu ya bei ya korosho kuwa ndogo.
Mhe. Majaliwa amewaambia wananchi hao kuwa bei imeshindwa kufikia Tsh.2,500 kwa kilo moja kutokana na kutofika kwa meli bandari ya mtwara suala linalolalamikiwa na wanunuzi wa zao hilo kukwamisha usafilishaji wa mizigo ya korosho za wakulima wa Lindi na Mtwara.
Hata hivyo, Mhe. Majaliwa amewaondoa hofu wakulima akiwaeleza kuwa Serikali imekutana na wamiliki wa meli na kuzungumza nao ambapo tayari wamekubali kupeleka meli bandari ya Mtwara, jambo ambalo litaleta matumaini ya wakulima katika uboreshaji wa bei ya kununulia korosho.
“ Ndugu wakulima msikate tamaa, endeleeni na kilimo kwani korosho bado inahitajika duniani……na mpaka kufikia tarehe 10 Novemba 2021 mabadiliko ya bei yataanza kuonekana”. Amesema Waziri Mkuu Mhe. Mjaliwa.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanya maamuzi ya usafirishaji wa korosho za Lindi na Mtwara kupitia bandari ya Mtwara badala ya bandari ya Dar es salaam, lengo likiwa ni kuendeleza bandari hiyo ingawa kumeibuka changamoto za biashara ya korosho ambayo serikali inaendelea kuishughulikia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.