Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameoneshwa kufurahishwa na huduma za afya zinazotolewa katika Halmashauri za Kilwa na Manispaa ya Lindi zilizopo Mkoa wa Lindi.
Waziri Ummy ameonesha furaha hiyo jana jumatano na Leo alhamisi alipofanya ziara ya kukagua huduma za afya na upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa ya kinyonga , Zahanati ya Nangurukuru na vituo vitatu vya afya vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Akizungumza na watumishi wa vituo hivyo baada ya kufanya zoezi la ukaguzi, amesema ameridhishwa na namna watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilwa na Zahanati ya Nangurukuru wanavyowahudumia wagonjwa.
Kipekee amefurahishwa na wahudumu katika wodi ya mama na mtoto, hospitali ya wilaya Kilwa kwa namna walivyo na weledi wa kufanya kazi yao kwa uelewa, upendo na upole.
Akihitimisha ziara yake ngazi ya halmashauri Leo alhamisi katika kituo cha afya cha mjini baada ya kufanya ukaguzi katika vituo vitatu vya afya vya Manispaa ya Lindi, ametoa pongezi kwa watumishi kwa kujituma kuwatumikia wananchi pamoja na changamoto ya uchache wao.
Pamoja na changamoto ya watumishi, amewasihi kuendelea kuwahudumia wagonjwa Kwa kuzingatia ubora wakati serikali inaendelea kushughulikia changamoto hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.