Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mradi wa FORVAC unaodhaminiwa na Serikali ya Finland umetoa vifaa vya uongezaji thamani wa mazao ya misitu kwa vikundi 20 kutoka vijiji 11 vya Wilaya ya Liwale.
Tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo lilifanyika jumamosi, tarehe 26 Juni 2021 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale ambapo zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo lilifanywa na Mhe. Judith Nguli ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo. Aidha, Vifaa vilivyotolewa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 108 ni pamoja na mizinga ya nyuki na vifaa vya kurinia asali, mashine za kuchana na kukereza mbao, mashine za kuchonga na kusafisha ubao, pikipiki za matairi matatu (guta sinoray 250 cc) kwa ajili ya kusafirishia mazao ya misitu.
FORVAC ni mradi wa uendelezaji mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu ambayo kwa Mkoa wa Lindi unatekelezwa katika Wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.