ZIARA YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA SHUGHULI ZA HUDUMA ZA AFYA YAFIKA KITUO CHA AFYA MJI- MANISPAA YA LINDI.-
Msisitizo Matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS katika utunzaji wa taarifa za kituo pamoja na udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya kituo.Mkurugenzi huduma za afya ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt.Rashid Mfaume amefanya ziara ya usimamizi shirikishi wa shughuli za huduma za afya Manispaa ya Lindi katika Kituo cha afya cha Mji (Town Health Centre) na kukagua hali ya utolewaji wa huduma za afya leo, Julai 15, 2024.Akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali wa afya kutoka Tamiseni, ngazi ya Mkoa wa Lindi (RHMT) na ngazi za wilaya za Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Lindi(CHMT) wamefanya ukaguzi wa huduma za afya zinazotolewa katika idara mbalimbali ikiwemo Kinywa na meno, Maabara, Bohari na Duka la dawa la kituo, Kliniki ya Baba, Mama na Mtoto pamoja na Wodi ya Wazazi.
Akizungumza baada ya kukagua utolewaji wa huduma katika Kituo hicho amewapongeza watumishi na wahudumu wa afya katika kituo hiko huku akiwataka watoa huduma za afya kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi kwa weledi, kuhakikisha wanatumia mfumo wa GoTHOMIS ili kuweza kutunza taarifa muhimu na kudhibiti ukusanyaji wa mapato, pamoja na kuhakikisha huduma zinazitolewa zinaboreshwa huku mazingira yake yakiwekwa vizuri ili kudhibiti magonjwa yasiende kwa wananchi kutokana na kuwa karibu sana na makazi ya watu.Aidha,ametoa maelekezo kwa vitu vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika ngazi ya halmashauri maeneo yake yapimwe na kupata hati miliki na kusisitiza ufanyikaji wa marekebisho ya vifaa kwa wakati ikiwemo magari ili yaweze kutumika katika kutoa huduma kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.