EQUIP Tanzania
Mpango wa Kuboresha Elimu Tanzania (EQUI- Tanzania) unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa maendeleo wa Uingereza, DFID. Mpango huu ni wa miaka minne ambao umeanza utekelezaji mwaka 2014 katika mikoa mitano hapa Tanzania yaani Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu na Tabora na ikaongezwa mikoa ya Lindi na Mara mwaka 2015. Jumla ya fedha Tsh 136 bilioni zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu kwa kipindi cha miaka minne.
Mpango huu unalenga kuongeza ubora wa elimu kwa shule za msingi unaozingatia jinsia. Mpango wa Kuboresha Elimu Tanzania unatarajia kuwafikia zaidi ya wanafunzi milioni mbili na zaidi ya walimu 49,000 waliopo shule 4,452, kata 1,123 zilizopo kwenye halmashauri 51 ndani ya mikoa saba ya mpango huu.
Katika ngazi ya mkoa mpango huu unasimamiwa na Katibu Tawala wa mkoa akisaidiwa na watendaji wa sekretarieti ya mkoa. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa elimu katika ngazi ya halmashauri. Hivyo watendaji wa halmashauri, waratibu elimu kata na walimu wakuu ndiyo watekelezaji wa shughuli zilizopangwa katika program hii kwa kushirikiana na wazazi na asasi za kiraia.
Katika kufikia maono ya Taifa ya kuboresha elimu Tanzania, EQUIP- Tanzania ina malengo makuu yafuatayo:
Shughuli zifuatazo zimetekelezwa
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
- Pia walimu wote wamepata ujuzi na maarifa ya jinsi ya kulitawala darasa wakati wa ufundishaji kwa kuzingatia jinsia (Gender Responsiveness).
Wasimamizi wakuu wa mafunzo haya ni wahadhiri wa chuo kikuu huria Tanzania na Taasisi ya Elimu Tanzania. Serikali inategemea kuwa wanafunzi wa darasa na kwanza na la pili wajengewe uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kabla hawajaingia darasa la tatu.
- Walimu wote wameweza kupata mafunzo ya jinsi ya kumfundisha mtoto/mwanafunzi jinsi ya kusoma, kuandika na kuhesabu. Mafunzo haya yamewezeshwa na wakufunzi toka vyuo vya ualimu Nachingwea, Mtwara na Kitangali.
EQUIP -Tanzania.
Pia wamefundishwa jinsi ya kutumia fedha ya ruzuku ya pikipiki ambayo wanapewa kila mwezi fedha zisizozidi Tsh 210,000 kwa ajili ya matengenezo ya pikipiki, mafuta na utawala akiwa kazini. Ni imani ya serikali kuwa walimu wakuu watakuwa mahiri katika kuongoza shule na waratibu elimu kata watasimamia kwa ukaribu shule zilizopo kwenye kata zao kwa kutumia uwezeshwaji uliofanywa na serikali chini ya program ya
Waratibu elimu kata wamepewa mafunzo ya jinsi ya kutumia pikipiki walizokabidhiwa na serikali kwa ajili ya kusimamia shughuli za elimu katika kata zao.
Mpango wa EQUIP-Tanzania umewawezesha kutambua sifa za shule mahiri, mwalimu mkuu/mratibu elimu kata mahiri, umahiri wa jinsi ya kuandaa mpango mkakati wa maendeleo ya shule, jinsi ya kuandika andiko mradi kwa maendeleo ya shule, umuhimu na kazi ya kamati ya shule, jinsi ya kuendesha kikao cha walimu cha kila wiki, na usimamizi na uongozi wa shule.
Viongozi hawa pia wamehusishwa kwenye mafunzo mengi ambayo yamewezeshwa kwa walimu ili wapate uelewa wa shughuli zinazofanyika na wazisimamie kwa ufanisi mkubwa. Wakurugenzi na wahasibu wamewezeshwa kwenye eneo la usimamizi wa fedha na kutoa ripoti ya matumizi ya fedha kila mwezi na kila muhula. Serikali inauhakika shughuli zote zilizopangwa kwenye program ya EQUIP-Tanzania zitasimamiwa vizuri na mkoa husika.
Viongozi wa mkoa wakiwemo katibu tawala wa mkoa, maafisa mipango, wakurugenzi, wahasibu, wakaguzi wa mahesabu wa ndani, maafisa maendeleo, maafisa elimu, wamewezesha kwa kupata mafunzo ya jinsi ya kuandaa mpango mkakati wa mkoa na wilaya kwa kuipa elimu kipaumbele kama dira ya maendeleo ya Taifa 2025 inavyoelekeza.
Pia shule imepewa mbao ya matangazo ambapo shughuli zinazoendeshwa shuleni ziwe wazi kwa wananchi. Kwa ushirikiano huu ni imani ya serikali kwamba jamii zitakuwa karibu na shule kwa maendeleo ya jamii husika
Kila Halmashauri imetengewa Tsh 10 million kwa muhula ili kusambaza taarifa za mafanikio kwa njia ya simulizi kwa jamii inayoizunguka.
Nusu ya idadi ya shule za mkoa wa Lindi watapokea Tsh 1,500,000 kila shule kwa ajili ya kuendesha shughuli za uzalishaji ili kuitegemeza shule na wanafunzi wajifunze elimu ya kujitegemea. Hivyo shule itakuwa na miradi ya uzalishaji inayoongozwa na wanafunzi, walimu na jamii.
Pia kila shule imeunda umoja wa wazazi na walimu ambapo kila darasa limewakilishwa na wazazi wawili wenye watoto katika darasa husika. Hivyo wazazi hao watakuwa wafuatiliaji wa karibu kwa kila siku katika darasa husika. Umoja huu umewezeshwa kiasi cha shilingi 550,000 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na uhamasishaji kwa wanafunzi juu ya kujifunza. kamati za shule zimepewa mafunzo ya jinsi ya kusimamia shule kwa ukaribu na umuhimu wa uwepo wao kisheria.
Mpango wa EQUIP- Tanzania umewezesha jamii kuelewa na kujenga uwezo wa kuwa na mipango ya kuisaidia shule kutatua changamoto mbalimbali watakazozibaini kwa kushirikiana na uongozi wa shule. Kwa kutumia Asasi za Kiraia, kila kijiji kimeunda kikosi kazi cha kusimamia katika kupanga na kutekeleza vipaumbele vya elimu katika maeneo yao.
SN |
LGA
|
1st,Tranhe |
2nd,Tranche |
3rd,Tranche |
4th,Tranche |
Total |
1 |
Liwale DC
|
265,078,388
|
295,582,575
|
231,382,549
|
235,001,007
|
1,027,044,519
|
2 |
Lindi DC
|
500,521,416
|
554,689,963
|
429,782,548
|
399,705,583
|
1,884,699,510
|
3 |
Lindi MC
|
163,446,185
|
181,924,440
|
127,861,929
|
147,778,768
|
621,011,322
|
4 |
Ruangwa DC
|
396,915,485
|
447,935,205
|
310,281,619
|
297,803,483
|
1,452,935,792
|
5 |
Nachingwea DC
|
465,642,421
|
519,689,963
|
407,064,744
|
377,716,595
|
1,770,113,723
|
6 |
Kilwa DC
|
458,326,867
|
511,356,233
|
376,636,811
|
356,018,852
|
1,702,338,763
|
7 |
|
|
|
|
|
|
|
JUMLA KUU
|
2,249,930,762
|
2,511,178,379
|
1,883,010,200
|
1,814,024,288
|
8,458,143,629
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.