Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akizundua uwanja wa mpira wa miguu unaoitwa Majaliwa Stadium uliopo wilayani Ruangwa. Kushoto kwake ni Mama Merry Majaliwa na kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki tukio hilo. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi)
Mhe. Godfrey W. Zambi akizungumza na wakazi wa manispaa ya Lindi waliokuwa wamefika kwenye uzinduzi wa kampeni ya TTCL Mpya ya Rudi Nyumbani Kumenoga kwa mkoa wa Lindi uliofanyika katika uwanja wa Ilulu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Katibu Tawala Mkoa, Bi. Rehema Madenge akiongoza kikao cha kazi cha wataalam (wakuu wa sehemu na vitengo) wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ofisini kwake. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akiwa ameketi katika kiti cha jamii ya watu wa pwani wakati katika kijiji cha makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam alipokwenda kufungua maonyesho ya tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Lindi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi)
Mhe. Godfrey W. Zambi (aliyesimama kushoto kwa bango) akipiga makofi baada ya kuzindua kampani ya kupunguza/kuzuia mimba za utotoni inayojulikana kwa jina la "Tumsaidie Akue Asome Mimba Baadae" uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili Manispaa ya Lindi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Picha ya pamoja ya viongozi wa halmahsauri na mkoa wa Lindi walioshiriki Semina ya Uraghibishi na Uhamasishaji kuhusu Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele. Semina hii ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Lindi na washiriki wake walikuwa ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, REO, RMO, Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Shirika la Ima World Health, Waratibu wa NTD na Waratibu wa Afya Shuleni. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi).
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Christopher Ngubiagai akijiandaa kupanda mti katika siku ya upandaji miti ambayo kimkoa ilifanyika wilayani Kilwa. kushoto kwake aliyesimama (amevaa kofia) ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Dkt. Bora Haule, na Mwenyekiri wa Halmashauri ya Kilwa, Mhe. Abuu Mjaka.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ilulu iliyopo wilayani Kilwa. Mhe. Zambi alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi na walimu kwa shule kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha sita 2019. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi).
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey W. Zambi akiongoza kikao kilichojadili tatizo la mimba za utotoni kwa mkoa wa Lindi. Kulia kwake ni Katibu tawala mkoa, Bi. Rehema Madenge na kushoto kwake ni Hakimu mkazi mfawidhi, Mhe. James Karayemaha. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa, kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, wilaya na halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akitoa maelekezo mbalimbali wakati alipokagua hali za barabara za mkoa wa Lindi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyeesha. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi).
Benki ya CRDB yatoa msaada wa mbegu za mahindi kilo 4000 kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko mkoani Lindi.
Baadhi ya watumishi wa serikali wilayani Nachingwea wakiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya mkuu wa mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi (hayupo pichani) ambapo alitoa maelekezo mbalimbali. (Picha na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi).
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akisikiliza maelezo ya namna ya utengenezaji wa barabara kutoka kwa mmoja wa wanakikundi waliohitimu mafunzo hayo. Mafunzo hayo yameratibiwa na halmashauri ya Nachingwea kwa kushirikiana na chuo cha chuo cha teknolojia stahiki ya nguvu kazi (ATTI). (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.