Mhe. Zambi aitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuhakikisha inalipa deni la fedha za mikopo ya vijana, wanawake na walemavu inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani. Hii ni baada ya mkaguzi wa nje mkoa wa lindi kuwasilisha madeni ya fedha hizo za mikopo.
Mhe. Zambi amewahakikishia wajumbe wa baraza maalum la madiwani wilayani Kilwa kuwa vifungashio vya zao la ufuta vipo vya kutosha katika Chama Kikuu cha Lindi Mwambao na hivyo amewataka watendaji wahakikishe AMCOS zinapatiwa vifungashio hivyo bila usumbufu wowote.
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.