Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amefungua kikao kazi cha tathmini ya robo mwaka dhidi ya ugonjwa wa vikope (TRAKOMA) kilichoandaliwa na Shirika la Sightsavers kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Mkoa.
Jaji (Mst.) Thomas Mihayo amewataka maafisa waandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kuhakikisha wanasimamia vizuri zoezi hilo ili likamilike kama lilivyokusudiwa. Hayo ameyasema baada ya kufungua mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi wa Halmashauri na Maafisa TEHAMA.
Mhe. Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi azungumza na viongozi wa Lindi kuhusu mafunzo na zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa mkoa wa Lindi.
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.